Nyumba ya Familia ya Onni & Ilona ni eneo la mkutano lililokubaliwa kwa familia zote. Wafanyikazi wetu hapa husaidia na kuongoza wageni na kuhakikisha kuwa kila kitu kinaendelea vizuri. Mbali na Kifini, wafanyakazi wetu wanazungumza Kiingereza na pia wanajua kuwasiliana kwa lugha ya ishara. Utawatambua wafanyakazi wetu kwa ishara wanayoibeba.

Katika Nyumba ya Familia ya Onni & Ilona, unaweza kukutana na familia zingine, watoto wako wanaweza kucheza, unaweza beba na kula chakula chako mwenyewe na utapata kikombe cha kahawa na chai kwa bei nafuu. Watoto wako katika Nyumba ya Familia kwa wajibu wa wazazi wao. Familia husafisha na huhakikisha  midoli yote imerudishwa mahali inafaa. Kutembelea na shughuli za Nyumba ya Familia ni bure. Unaweza pia kushiriki katika makusanyiko au mipango mbalimbali ambayo imeandaliwa katika vyumba hivi. Soma ratiba ya Nyumba ya Familia kila wiki kupata ujumbe kuhusu shughuli na mipango hii.

 

Anwani ya Nyumba ya Familia ya Onni & Ilona ni: Pohjolankatu 6 L6, 74100 Iisalmi.

 

Nyumba ya Familia ya Onni & Ilona imefunguliwa Jumatatu hadi Ijumaa masaa ya 0900 - 1400.

 

Umekaribishwa kujiunga nasi kwenye Nyumba ya Familia!